• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wanonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-07-20 20:00:17

    Wawekezaji wa Shirikisho la Madini ya Granite India wameonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya uongezaji thamani madini ya mawe yenye thamani ya granite na mable nchini Tanzania.

    Wawekezaji hao walionesha nia hiyo walipokutana na kuzungumza na Waziri wa Madini, Angella Kairuki Jijini Dar es Salaam.

    Waziri Kairuki aliueleza ujumbe huo kuhusu azma ya Tanzania kukaribisha wawekezaji katika ujenzi wa vinu vya kuyeyusha madini ya metali, usonara na ukataji na ung'arishaji madini ya vito hususan Tanzanite ambayo kwa kiasi kikubwa husafirishwa nje yakiwa ghafi.

    Waziri Kairuki amewashauri wawekezaji hao kukutana na uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ili kuona namna bora ya kushirikiana katika miradi mbalimbali ikiwemo ya mawe ya thamani, bati na madini mengine.

    Aliwataka wawekezaji hao kuona wanavyoweza kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini nchini hasa katika masuala ya masoko na mitaji.

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Madini ya Granite na sekta ya mawe India, Keshava Murthy amesema wako tayari kuwekeza kwenye madini ya granite pamoja na marble kwa kuanza na makontena kati ya 20 hadi 50 kwa mwezi.

    Murthy amesema shirikisho hilo lina wanachama 1,200 wanaojihusisha na shughuli za uongezaji thamani madini ya granite nchini humo.

    Kuhusu ushirikiano na Stamico, Murthy aliahidi shirikisho hilo litakutana na Stamico kwa lengo la kubadilishana ujuzi, ikiwemo kuangalia namna bora ya kushirikiana katika sekta husika.

    Mbali ya Waziri Kairuki, wawekezaji hao watakutana na Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania, kutembelea Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na maeneo yenye uchimbaji wa granite Dodoma.

    Wawekezaji hao pia walitembelea nchi za Namibia, Zimbabwe na Malawi kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji katika madini hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako