• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 14-Julai 20)

  (GMT+08:00) 2018-07-20 20:19:54

  Serikali yachukua hatua kuokoa sekta yha sukari

  Sekta ya sukari nchini Tanzania imekuwa ikikabiriwa na changamoto kadhaa ambazo zimeilazimu Serikali na wadau kuchukua hatua kila mara.

  Takwimu za Serikali zinaonyesha mahitaji ya sukari nchini Tanzania ni tani 630,000 kwa mwaka ambazo kati yake, tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 145,000 ni malighafi viwandani.

  Licha ya kuwapo kwa wazalishaji wa ndani, wanaowashirikisha wakulima wadogo, uzalishaji bado hautoshi. Mabadiliko ya tabianchi na sababu nyinginezo bado zimeendelea kuwa kikwazo cha Tanzania kujitegemea kwa mahitaji yake ya bidhaa hiyo.

  Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema ukame uliozikumba nchi za ukanda wa mashariki, kati na kusini mwa Afrika mwaka 2017/18 umesababisha Tanzania kushindwa kuzalisha tani 314,000 na kupata tani 300,399 pekee.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako