• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wananchi wa UAE wafuatilia ziara ya rais Xi Jinping nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-07-20 22:04:11

    Rais Xi Jinping wa China yuko kwenye ziara ya kiserikali ya siku tatu kuanzia jana nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Hii ni mara kwanza kwa kiongozi wa China kuizuru nchi hiyo katika miaka 29 iliyopita, na ziara hiyo ina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Wananchi wa UAE wanafuatilia na kuisifu sana ziara hiyo ya rais Xi.

    "Hamjambo! Karibu rais wa China, mke wa rais pamoja na wageni wengine kutoka China kuitembelea nchi yetu nzuri Falme za Kiarabu! Tunaona fahari kubwa. China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa Falme za Kiarabu, na tuna matumaini makubwa kuwa urafiki kati ya nchi zetu utainuka na kufikia ngazi ya juu zaidi."

    Maneno hayo kwa lugha ya kichina yamesemwa na waziri wa mambo ya vijana na ulinzi wa Falme za Kiarabu Bw. Shama Al Mazroui, ambayo yameonesha ukarimu wa moyo wa dhati wa wananchi wa Falme za Kiarabu kwa rais Xi Jinping.

    Ziara ya rais Xi Jinping na mke wake Bibi. Peng Liyuan imepewa uzito mkubwa nchini Falme za Kiarabu. Waziri wa uchumi wa nchi hiyo Bw. Sultan Al Mansouri amesema, ziara hiyo ina umuhimu mkubwa, na imeonesha ishara muhimu kwa viongozi wa Falme za Kiarabu kuwa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni muhimu sana kwa pande zote mbili. Falme za Kiarabu siku zote inaheshimu sana China, ambalo ni kundi muhimu tena kubwa la uchumi, na imetoa uzoefu mwingi katika kujiendeleza. Amesema ziara ya rais Xi wa China imepata mafanikio mengi muhimu, na anaamini kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za siasa, uchumi na jamii utazidi kuimarishwa katika siku za baadaye.

    Mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Falme za Kiarabu Bw. Khalifa Abdullah ambaye pia mwanataaluma wa masuala ya kichina, hivi sasa anashughulikia utafiti kuhusu uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Beijing. Anasema ziara ya rais Xi Jinping nchini Falme za Kiarabu si kama tu imeongeza kiwango cha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, bali pia itazidi kuimarisha uratibu kati ya nchi hizo katika mambo ya kikanda na ya kimataifa.

    Wakati wa ziara hiyo, mrithi wa mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amemtunukia rais Xi Jinping medali ya Zyed ambayo ni heshima ya kiwango cha juu ya Falme za Kiarabu. Pia amemzawadia rais Xi farasi aina ya kiarabu ambaye ni wa kale tena wa thamani kubwa duniani, hatua ambayo imeonesha nidhamu ya kiwango cha juu kutoka Ufalme wa Falme za Kiarabu kwa rais Xi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako