• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Senegal waahidi kuleta mustakabali mzuri wa uhusiano wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-07-22 08:28:23
    Rais Xi Jinping wa China na rais wa Senegal Macky Sall wamekutana jana (jumamosi) katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

    Katika mazungumzo yao marais hao wamekubaliana kufanya juhudi kwa pamoja ili kuleta mustakabali mzuri wa uhusiano wa nchi hizo mbili, pia walishuhudia kusainiwa kwa mapatano kadhaa ya ushirikiano yakiwemo yanayohusu ujenzi wa pamoja wa "Ukanda mmoja na Njia moja".

    Katika mazungumzo hayo, Rais Sall alieleza kuridhia uhusiano kati ya Senegal na China uliojengwa kwa msingi wa mshikamano, uaminifu, heshima na kunufaishana, na kusema Senegal inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na inapenda kushiriki kwenye ujenzi wa miundombinu inayorahisisha mawasiliano kati ya nchi tofauti. Ameongeza kuwa, Baraza la ushirikiano wa China na Afrika ni mfumo wenye ufanisi, mshikamano unaoshirikisha pande mbalimbali, na limeanzishwa kwa msingi wa ushirikiano wa mambo halisi, na ni kwa sababu hiyo Senegal inaunga mkono kuimarisha baraza hilo.

    Naye rais Xi Jinping alimpongeza rais Sall kwa kutilia maanani uhusiano kati ya China na Senegal, kuitikia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuchangia kazi ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesisitiza kuwa China inaunga mkono juhudi za Senegal katika kuimarisha uwezo wake wa kupambana na ugaidi, na kudumisha utulivu na amani.

    Kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika, rais Xi Jinping amesema anatilia maanani uhusiano huo, kwani pande hizo mbili ni marafiki wa muda mrefu zenye hatma ya pamoja. Amesema maendeleo ya China yanaipa Afrika fursa nyingi huku maendeleo ya Afrika yana uwezo wa kuongeza kasi ya maendeleo ya China. Ameongeza kuwa mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika utafanyika jijini Beijing mwezi Septemba, ambapo anatarajia kukutana na viongozi wa nchi za Afrika na kujadili mpango wa ushirikiano wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako