• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Brexit asema makubaliano ya mpango wa Uingereza kujiondoa EU yatafikiwa mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2018-07-22 19:35:04

    Waziri mpya wa Uingereza anayeshughulikia Mpango wa Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya BREXIT, Bw. Dominic Raab amezungumza kupitia BBC kuwa mpango wa nchi yake kujitoa huenda ukaafikiwa mwezi Oktoba mwaka huu.

    Katika hatua nyingine, Waziri huyo pia alisisitiza kuwa nchi yake pia inajiandaa kupokea matokeo ya kushindikana kwa mpango huo.

    Aidha waziri huyo amesema, alhamisi hii anatarajia kwenda Brussels nchini Ubeligiji kwa ajili ya mazungumzo na kuona uwezekano wa kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.

    Mpaka sasa Uingereza imepanga kujiondoa rasmi katika Umoja wa Ulaya EU mnamo Machi 29 mwaka 2019, licha ya kuwa pande hizo mbili bado hazijakubaliana namna ya kushughulikia masuala ya biashara baada ya kuachana.

    Lakini Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May ameeleza matumaini kuwa mpango mpya wa serikali yake utaziwezesha pande mbili hizo kufikia makubaliano kuhusu uhusiano kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako