• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia laharibu ngome za al-Shabaab kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-07-23 07:14:22
    Kamanda wa Jeshi la Somalia Mohamed Mohamud Gutale amesema Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) limeharibu ngome za kundi la al-Shabaab karibu na mji wa Qoryoley katika mji wa Shabelle ya chini, kusini mwa Somalia.
    Bw. Mohamed ameiambia redio inayomilikiwa na serikali kwamba operesheni ya kijeshi ililenga ngome za wanamgambo na kufanikiwa kuteketeza vifaa vya magaidi. Hadi sasa hajaeleza idadi ya wapiganaji waliokamatwa wakati wa operesheni hiyo au idadi ya majeruhi kwa upande wa SNA na kama walikuwepo washirika wa kimataifa waliokuwa wakishirikiana nao katika operesheni hiyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako