• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Nigeria lazuia shambulizi la Boko Haram katika mkoa wa Yobe

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:08:46

    Jeshi la Nigeria limesema limefanikiwa kuzuia shambulizi dhidi ya kikosi kilichokuwa kwenye doria, ambalo liliratibiwa na waasi wa Boko Haram katika jamii ya Sasawa kaskazini mashariki mwa Yobe.

    Kwenye taarifa yake msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Texas Chukwu, amesema wakati wakizuia shambulizi hilo jeshi la Nigeria limewauawa wengi wa waasi hao, na kwamba ripoti zinaonesha kuwa waasi, ambao mpango wao wa awali ni kushambulia na kupora soko la Babbangida, waliacha mpango wao na badala yake kuvamia wanajeshi waliokuwa kwenye doria. Kwa mujibu wa msemaji huyo, wanajeshi kadhaa wamejeruhiwa na hatimaye hali ilidhibitiwa.

    Kundi la Boko Harama limekuwa likilaumiwa kwa vifo vya watu zaidi ya elfu 20, na kusababisha watu milioni 2.3 kikimbia makazi yao nchini Nigeria tangu mwaka 2009.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako