• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi ya Ethiopia yakamata watuhumiwa 18 wanaoingiza silaha, na kuhamisha fedha za kigeni kwa njia haramu

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:09:24

    Kamisheni ya Polisi nchini Ethiopia imesema imewakamata watuhumiwa 18 wakihusishwa na kuingiza silaha nchini humo pamoja na kuhamisha fedha za kigeni kwa njia haramu.

    Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja kufuatia madai ya hivi karibuni ya nchi hiyo kwamba silaha zinaingizwa kiharamu nchini humo, ambazo zinasemekana kuleta athari kubwa ya amani na usalama nchini.

    Serikali ya Ethiopia pia hivi sasa inapambana kuondoa upungufu wa fedha za kigeni, ambazo zimekuwa zikilemaza uchumi wa nchi katika miaka ya hivi karibuni.

    Jumamosi polisi walitangza kukamata zaidi ya dola milioni 10 za Marekani ambazo zilikuwa zikitolewa kiharamu nje ya Ethiopia katika siku chache.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako