• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa IMF asema kuongezeka kwa ushuru kutahujumu uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:34:12

    Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani IMF Bibi Christine Lagarde amesisitiza hatari inayotokana na sera za kujilinda kibiashara kwa uchumi wa dunia.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumamosi huko Buenos Aires, nchini Argentina, Bibi Lagarde alitaja makadirio mpya kuhusu pato la jumla la dunia baada ya Marekani kutoza ushuru mkubwa kwa bidhaa nyingi zinazoagizwa kutoka nchi nyingine, na kusema uchumi wa dunia utaweza kushuka kwa asilimia 0.5 ifikapo mwaka 2020, endapo Marekani itatekeleza ushuru wote kama ilivyotishia kuutoza.

    Bibi Lagarde amesema uchumi wa Marekani pia utapata hasara zisizoepukana kutokana na sera zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako