• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 11 wauawa na wengine 14 wajeruhiwa kwenye shambulizi la kujitoa muhanga Kabul

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:34:37

    Watu 11 wameuawa na wengine 14 wamejeruhiwa kwenye shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea jana mjini Kabul, Afghanistan.

    Msemaji wa polisi nchini humo Bw. Hashmat Stanikzai amesema shambulizi hilo limetokea saa 11 jana jioni kwenye barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul, wakati msafara wa magari ya makamu wa kwanza wa rais wa Afghanistan jenerali Abdul Rashid Dostum ulipokuwa unapita kwenye eneo hilo.

    Wahanga wote wa tukio hilo ni raia wa kawaida na maofisa wa polisi, na majeruhi 48 wote wamekimbizwa hospitali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako