• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Russia wajadili kwa njia ya simu kuhusu matokeo ya mkutano wa Helsinki

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:35:18

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Bw. Sergey Lavrov, na kujadili matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano wa marais wa nchi mbili uliofanyika Helsinki, na masuala mengine wanayofuatilia kwa pamoja.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bibi Heather Nauert, kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika Jumamosi, mawaziri hao wamejadiliana kuhusu matunda yaliyopatikana kwenye mkutano wa Helsinki, na masuala mengine ya kimataifa, likiwemo suala la Syria.

    Kabla ya hapo, balozi wa Russia nchini Marekani Bw. Antoly Antonov alisema Ijumaa kuwa nchi yake iko wazi kwa mkutano mwingine kati ya marais wa nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako