• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la majini la Libya lakanusha shutuma za kupuuza uokoaji wa wahamiaji

    (GMT+08:00) 2018-07-23 09:35:34

    Jeshi la majini la Libya limekanusha shutuma zilizotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Hispania za kupuuza kazi ya kumwokoa mhamiji mmoja mwanamke na kuokota miili ya wahamiaji wengine wawili kutoka kwenye boti moja iliyozama pwani ya Libya.

    Shirika hilo liitwalo "Proactiva Open Arms" limekishutumu kikosi cha walinzi wa pwani cha Libya kumwacha mwanamke aliye hai na miili ya mwanamke mwingine na mtoto kwenye boti moja ya wahamiaji haramu iliyozama.

    Jeshi la majini la Libya limekanusha shutuma hizo na kuzitaja kuwa ni uongo na kusema ni sehemu ya kampeni ya shirika hilo dhidi ya walinzi wa pwani ambao wanaona ni maadui wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako