• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakosoa kitendo cha Vipers kuachana na kocha Miguel

    (GMT+08:00) 2018-07-23 11:18:37

    Wadau wa michezo nchini Uganda wameeleza hofu yao juu ya kitendo cha timu ya Vipers SC kumfukuza kazi kocha wake Miguel Da Costa, wakati huu ambapo timu hiyo inajiandaa na mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa msimu ujao.

    Wengi wamesema kuwa, hata kama kuna kasoro zilizojitokeza ni vyema zingetatuliwa kuliko kumtimua kocha huyo ambaye ameipa ubingwa wa ligi kuu klabu hiyo msimu huu.

    Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo Abdul Wasike, Vipers imeamua kuachana na Miguel kutokana na mabadiliko ya kawaida tu na sasa msaidizi wake Mosses Golola atachukua wadhifa huo kwa muda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako