• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sakata la kustaafu timu ya Taifa ya Ujerumani laishtua dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-23 11:19:15

    Mchezaji wa soka Mesuit Ozil ameandika kuwa anajihisi kuwa hahitajiki tena, na anafikiri mchango alioutoa kwenye timu ya taifa tangu ajiunge nayo mwaka 2009 umesahaulika, na hii ndiyo sababu ya yeye kuamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani wakati bado umri wake unaruhusu kucheza.

    Sababu nyingine ambayo wachambuzi wa masuala ya michezo wameendelea kuifafanua ni kwamba kile kitendo cha kibaguzi kilichoonyeshwa na chama cha mpira cha Ujerumani DFB, huenda kimechangia kwa kiasi kikubwa.

    DFB inadaiwa kumhoji Ozil na kumtaka aandike barua ya kujieleza ni kwa nini alipiga picha na Rais wa Uturuki Recep-Tayyip Erdogan siku chache kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia, huku yeye akijibu kuwa kitendo cha yeye kukutana na Erdogan hakikuwa na uhusiano wowote na masuala ya kisiasa.

    Lakini mwenyewe Ozil anadai kusikitishwa zaidi na kitendo cha DFB kumshinikiza kocha Joachim Low kumuondoa kwenye kikosi kilichotarajiwa kushiriki kombe la dunia, pamoja na lawama zilizojitokeza baada ya kocha huyo kukaidi na kumtumia.

    Ozil anasemekana kuandamwa na vitendo vya kibaguzi kutokana na kuwa na asili ya wazazi wawili, mmoja kutoka ujerumani na mwingine kutoka uturuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako