• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni nani anayedhibiti mpira wa vita ya kibiashara duniani?

    (GMT+08:00) 2018-07-23 13:43:47

    Mkutano wa mawaziri wa fedha na wakuu wa benki kuu wa nchi za kundi la G20 umefungwa jijini Buenos Aires, Argentina ambapo suala la biashara limefuatiliwa zaidi.

    Tangu mwanzoni mwa Machi Marekani ilianza kutekeleza uamuzi wa kuongeza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminium kutoka China, na kuchochea vita ya kibiashara dhidi ya China. Kwa upande mmoja Marekani inaziwekea majukumu ya kutatua mvutano wa kibiashara China na Umoja wa Ulaya, ambazo ni wenzi wake wakubwa wa kibiashara, huku ikijidai kuwa ndio nchi inayoathiriwa zaidi, na kusema mpira wa kutatua suala lililopo upo kwa China, Umoja wa Ulaya na pande nyinginezo. Katika upande mwingine, Marekani ilichukua hatua moja baada ya nyingine kabla ya pande nyingine, kwa kupitia kuongeza ushuru wa forodha. Sababu pekee ni kwamba, Marekani haitaki vita hiyo ya biashara kwisha. Mbali na hayo, inataka kudhibiti vita hiyo kwa kufuata kanuni yake, njia yake, na kuiendeleza vita hiyo.

    Ingawa Umoja wa Ulaya bado unashikilia kuwa ni mshirika wa Marekani, lakini ni washirika sio mkuu washiriki, waziri wa fedha wa Ufaransa Bw. Bruno Le Maire amesema kwenye mkutano huo wa G20 kuwa, Marekani inapswa kuheshimu kanuni ya biashara ya pande nyingi, kutatua mvutano kati yake na Umoja wa Ulaya na China kwa njia ya mazungumzo. Lakini hatujui kama serikali ya Marekani inasikia hilo au la.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako