• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atuma pongezi kwa Mkutano wa tano wa Baraza la Watu kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-23 14:35:03

    Mkutano wa tano wa Baraza la Watu kati ya China na Afrika umefanyika leo mjini Chengdu, kusini magharibi mwa China. Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa mkutano huo.

    Kwenye salamu zake rais Xi amesema Baraza la watu kati ya China na Afrika likiwa ni daraja muhimu kati ya watu wa China na Afrika, limetoa mchango mkubwa katika kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa pande hizo mbili tangu lilipoanzishwa mwezi Agosti mwaka 2011.

    Rais Xi amesisitiza kuwa urafiki kati ya watu ni msingi muhimu wa uhusiano kati ya nchi, na pia ni nyanja muhimu ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika katika siku zijazo. Amewataka washiriki wa mkutano huo wabadilishane mawazo na uzoefu, na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika, ili kuimarisha msingi wa umma na kutia msukumo mpya katika ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako