• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Ziara ya Rais Xi Jinping kuleta mafanikio makubwa ya uchumi

    (GMT+08:00) 2018-07-23 18:43:28
    Rais wa jamhuri ya Demokrasia China Xi Jinping amewasili nchini Rwanda, kwenye ziara yake ya kwanza nchini humo.

    Rais Xi amekutana na rais wa Rwanda Paul Kagame jijini Kigali, na atafanya ziara ya siku mbili nchini humo itakayohusisha ushirikiano wa sekta mbali mbali za uchumi na maendeleo.

    Waziri wa ushirikiano wa kimataifa Olivier Nduhungirehe amesema ziara ya kiongozi wa China Xi Jinping ni inalenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili .

    Marais hao wawili Kagame watasaini mikataba 15 kabla kiongozi huyo kutamatisha ziara yake.

    Waziri Nduhungirehe pia amesema mataifa hayo mawili yatasaini pia makubaliano ya upanuzi wa hospitali ya Masaka,ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa Bugesera na Jiolojia.

    Xi Jinping amefika Rwanda baada ya kufika nchini Senegal na kutia saini mikataba 15 ya kibiashara.

    Baada ya ziara yake nchini Rwanda Rais Xi Jinping ataelekea nchini Afrika kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako