• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika Kusini zafanya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2018-07-23 19:00:17

    Wakati China na Afrika Kusini zikiwa zinatimiza miaka 20 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi, Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng hivi karibuni alisema kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizi mbili umeendelea vizuri kwa pande zote na katika sekta mbalimbali.

    Bw. Gao Feng alisema China na Afrika Kusini ni marafiki muhimu ya biashara. Katika mwaka 2017, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola za kimarekani bilioni 39.17 na kuongezeka kwa asilimia 11.7 kuliko mwaka 2016 wakati kama huu.

    Aidha makampuni ya China yaliwekeza dola za kimarekani bilioni 10 nchini Afrika Kusini katika sekta ya madini, reli, vyombo vya nyumbani, magari, fedha, ujenzi wa nyumba na kahawa, na njia ya uwekezaji ilibadilika na kuwa ya kununua hisa za makampuni wenyeji.

    Bw. Gao Feng ameongeza kuwa, China inapenda kufanya juhudi pamoja na Afrika Kusini kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwa pande zote ambao utakuwa mfano wa kuigwakwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako