• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya ajira iko tulivu kwa ujumla nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-23 19:09:10

    Msemaji wa idara ya nguvu kazi na huduma za jamii ya China Bw. Lu Aihong leo hapa Beijing amesema kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, hali ya ajira ni tulivu kwa ujumla.

    Bw. Lu amesema, "kwanza nafasi ya ajira katika maeneo ya mijini imeongezeka kwa kasi. Katika mwezi Januari hadi mwezi Juni, watu milioni 7.52 wamepata ajira mpya mijini, idadi hiyo imeongezeka kwa laki 1.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Hiki ni kigezo muhimu zaidi. Pili, kiasi cha watu waliopoteza ajira mijini kimedumu kuwa cha chini. Hadi mwishoni mwa robo ya pili ya mwaka huu, kiasi cha watu wanaopoteza ajira mijini kimefikia 3.83% kote nchini, na kushuka kwa asilimia 0.12 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Idara ya takwimu ya China imesema kuwa, kiasi cha watu wanaopoteza ajira mijini kimekuwa chini ya asilimia 5 kwa miezi mitatu mfululizo. "

    Wakati huo huo, kiwango cha upatikanaji wa ajira kwa wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu pia kiko sawa na cha miaka iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako