• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haiogopi Marekani kutoza ushuru kwa bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2018-07-23 19:58:41

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China haiogopi Marekani kutoza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 500.

    Bw. Geng Shuang amesema, kuhusu vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani, China inashikilia msimamo wa dhabiti na wa wazi, na iko tayari kukabiliana na vita hiyo kama ikihitaji, na China imeweka wazi msimamo huo mara kwa mara. Amesema China ina uwezo na nia ya kulinda maslahi ya watu wake, na kwamba Marekani inatakiwa kujizuia, na kutatua masuala husika kwa njia sahihi.

    Ijumaa iliyopita, rais Donald Trump wa Marekani alisema anataka kutoza ushuru kwa bidhaa zote kutoka China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 500.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako