• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya kesi ya kampuniya kutengeneza Chanjo ya Changsheng

    (GMT+08:00) 2018-07-23 20:19:21

    Rais Xi Jinping wa China leo ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya kesi ya Kampuni ya Kutengeneza Chanjo ya Changsheng.

    Rais Xi ambaye yupo ziarani barani Afrika amesema, kitendo cha shirika hilo kutengeneza chanjo bandia kinashangaza watu, na ni kibaya sana. Ameagiza idara husika kushughulikia kesi hiyo kwa makini, na kutoa adhabu kali kwa wahusika.

    Rais Xi amesisitiza kuwa kuhakikisha usalama wa dawa ni wajibu wa lazima wa serikali, ambayo inapaswa kutilia maanani zaidi afya ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako