• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu ya Marekani yasema Bolton atakutana na mwenzake wa Russia Agosti

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:19:24

    Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa mshauri wa usalama wa taifa Bw. John Bolton atakutana na mwenzake wa Russia mwezi Agosti, kufuatia mkutano kati ya rais Donald Trump wa Marekani na rais Vladimir Putin wa Russia uliofanyika Julai 16 mjini Helsinki.

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema makubaliano ya hakika ya pekee yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Helsinki ni kuwa maofisa wa usalama wa taifa wa Marekani na Russia wataendelea na mazungumzo ya kikazi, lakini hakudokeza ajenda, lengo na washiriki wengine wa mkutano ujao wa Bw.Bolton.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako