• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatma ya wakazi milioni 4 wa Uingereza na Ulaya wanaoishi katika upande mwingine bado haijajulikana

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:19:41

    Ripoti iliyotolewa na Kamati ya Brexit ya Baraza la makabwela imesema haki za raia zaidi ya milioni 4 wa Uingereza na Ulaya wanaoishi katika upande mwingine baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulay,a bado hazijaamuliwa. Kamati hiyo imetoa mwito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuweka bayana hatua zao za kuamua hadhi ya raia wa Uingereza wanaoishi katika nchi hizo baada ya Brexit, na pia imezitaka nchi wanachama wa Ulaya ikiwemo Uingereza, kutoa taarifa wazi kuhakikisha haki za raia wote wa Ulaya na Uingereza wanaoishi katika upande mwingine.

    Imefahamika kuwa raia wapatao milioni moja wa Uingereza wanaishi katika nchi za Ulaya, huku zaidi ya raia milioni tatu wa nchi za Umoja wa Ulaya wakiishi nchini Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako