• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU wautaja ukosefu wa habari kuwa kikwazo cha biashara ya ndani ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:34:14

    Umoja wa Afrika umesema, ukosefu wa habari kuhusu fursa za soko kati ya wafanyabiashara barani Afrika ni chanzo kikuu kinachokwamisha biashara ya ndani barani Afrika.

    Ofisa wa biashara na viwanda wa Umoja huo Bw. Albert Muchanga amesema, biashara ya ndani barani Afrika ni chini ya asilimia 18 ya biashara za jumla za Afrika, ambayo ni chini zaidi kwa kanda yoyote duniani.

    Bw. Muchanga amesema hayo katika mkutano wa biashara ya kielektroniki wa Umoja wa Afrika. Ameongeza kuwa wataendeleza uchunguzi katika nchi za Afrika kufuatilia na kutoa habari kuhusu bei za bidhaa na huduma ili kuchochea biashara ya ndani barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako