• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan amesema matumizi ya sekta ya afya yazidi bajeti ya serikali

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:47:28

    Rais Omar Al Bashir wa Sudan amesema matumizi ya serikali kwenye sekta ya afya, yamezidi makadirio yaliyopo kwenye bajeti ya serikali.

    Akiongea mjini Khartoum kwenye shughuli za uzinduzi wa usambazaji wa vifaa tiba kwa ajili ya msimu wa mvua, Rais Al Bashir amesisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya msimu wa mvua na kupambana na magonjwa yanayotokea kwenye msimu huo.

    Waziri wa Afya wa Sudan Bw Bahar Garada ameahidi kuwa kila jimbo la Sudan litapatiwa vifaa tiba, na kutoa matibabu ya bure kwa wananchi wote kupitia sera ya mfuko wa afya wa taifa.

    Amewataka magavana wote kuhakikisha kuwa wanagawa vifaa tiba kwa ufanisi ili kuwanufaisha wananchi. Vifaa tiba vinavyogawiwa kwa msimu huu ni pamoja na dawa, zahanati za dharura, magari ya wagonjwa, benki za damu na majokofu ya kuhifadhia chanjo, vyenye thamani ya dola milioni 26.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako