• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wazitaka nchi za Afrika kuweka kanuni za kuhimiza maendeleo ya biashara kwenye mtandao wa internet

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:48:18

    Umoja wa mataifa umezitaka nchi za Afrika kuweka kanuni zinazoweza kuhimiza biashara kwenye mtandao wa internet.

    Akiongea mjini Nairobi, Katibu mkuu wa Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa mataifa Bw. Mukhisa Kituyi, amesema bara la Afrika liko nyuma kwenye biashara ya mtandao wa internet, kutokana na kutokuwepo kwa mazingira yanayofaa.

    Bw Kituyi amesema Africa inahitaji kuendeleza sheria za manunuzi kwenye mitandao ya kijamii, ili wateja waweze kuiamini. Kwenye mkutano wa siku tatu wenye lengo la kuimarisha uelewa kuhusu hali ya biashara kwenye mtandao wa internet, fursa na changamoto zake, na kutumia uzoefu uliopatikana katika sehemu nyingine duniani.

    Bw. Kituyi amesema kanuni za kutosha za kuwalinda wateja wanaoagiza bidhaa kwa njia ya mtandao na njia nzuri za kusafirisha bidhaa zinazonunuliwa kwa njia ya mtandao, kutahimiza biashara kwenye mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako