• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa walaani mashambulizi dhidi ya watoa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:48:40

    Mashirika mawili ya Umoja wa mataifa yamelaani vikali mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa utoaji misaada na vifaa vyao nchini Sudan Kusini, katika mji wa Bunj wa mkoa wa Upper Nile.

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR na Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu OCHA, yamesema kwenye taarifa zao tofauti kuwa vurugu zilitokea baada ya maandamano ya amani ya vijana katika kaunti ya Maban kubadilika kuwa vurugu, na kusababisha uporaji na kuchomwa kwa majengo na magari ya mashirika ya misaada.

    Taarifa ya OCHA imesema wafanyakazi wa misaada wanajitolea na kuwa hatarini kuondoka maisha ya watu wanaoathiriwa na mgogoro wa Sudan Kusini, wanatakiwa kuwa huru kufanya kazi kwenye yoyote kwa kufuata sheria za nchi.

    UNHCR imesema vijana waliokuwa wanaandamana kwa amani kupinga kukosekana kwa ajira, walivamia eneo lake na la mashirika kumi ya misaada ya kufanya uporaji kwenye ofisi na makazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako