• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania aamuru kufunga mashirika ya umma yasiyo na faida

    (GMT+08:00) 2018-07-24 09:53:45

    Rais John Magufuli wa Tanzania ametoa amri ya kuyafunga mashirika yote ya umma yasiyo na faida, ambayo hayajaipatia serikali mapato kwa muda mrefu.

    Rais Magufuli amesema serikali imewekeza zaidi ya dola bilioni 21.5 za kimarekani kwa mashirika mengi, lakini serikali imepata mapato kidogo kutokana na uwekezaji huo. Amesema mashirika yote 90 yanatakiwa kuipatia serikali mapato kila mwaka, la sivyo yatafungwa.

    Baada ya Rais Magufuli kutoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam, serikali ya Tanzania imepata mapato ya dola milioni 319 za kimarekani kutoka mashirika 43 ndani ya muda mfupi. Rais Magufuli amesema mashirika hayo mengi hayafanyi kazi vizuri kutokana na utawala mbaya na ufisadi. Ameonya kuwa mashirika hayo yanafanya vitendo vya uvunjaji sheria katika kutangaza mali zao, faida, gharama za usimamizi na uendeshaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako