• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna wa haki za binadamu wa UM afuatilia hali ya Palestina

    (GMT+08:00) 2018-07-24 10:09:01

    Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya haki za binadamu ya wapalestina kutokana na matumizi ya kimabavu mpakani yaliyotokea hivi karibuni kati ya ukanda wa Gaza na Israel.

    Amesisitiza kuwa ni muhimu kutatua vyanzo vya maandamano ya hivi karibuni, yaani hali mbaya ya maisha huko Gaza.

    Habari nyingine zinasema, waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu jana huko Jerusalem alifanya mkutano na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov kuhusu msukosuko wa Gaza.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema pande hizo mbili zimejadili masuala ya kikanda na hali ya Gaza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako