• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo Rwanda: Kocha Rugambwa wa Mbio za Baiskeli afariki dunia

    (GMT+08:00) 2018-07-24 10:32:56

    Sekta ya michezo nchini Rwanda jana imepata pigo kufuatia taarifa za kifo cha Jean Batiste Rugambwa ambaye ni moja ya wadau waliopigania maendeleo ya mchezo wa mbio za baiskeli kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita, na kuifanya Rwanda sasa kuwa moja ya nchi zinazoshika nafasi za juu kwenye ubora wa mchezo huo duniani kwa sasa.

    Kifo chake kimesababishwa na ajali ya barabarani ambapo akiendesha pikipiki alipogongana na lori na umauti ukamkuta papo hapo.

    Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la mchezo wa mbio za baiskeli la Rwanda FERWACY, siku hiyo ya ajali, Jean alikuwa anarejea nyumbani baada ya kutoka kwenye mkutano wa FERWACY kukamilisha maandalizi ya mbio za mwaka huu za kimataifa za Rwanda zitakazofanyika mwezi Agosti, ambapo binafsi alihusika kushauri mtandao wa barabara zitakazotumika.

    Jean ambaye ni kocha mzoefu wa waendesha baiskeli na mwanzilishi wa timu yam bio za Baiskeli ya Les Amis Sportif de Rwamagana atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye mageuzi ya hivi sasa yaliyofanywa na shirikisho la mchezo wa mbio za baiskeli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako