• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lasaidia ushirikiano kati ya China na Afrika kuendelezwa kwa madhubuti

  (GMT+08:00) 2018-07-24 18:34:33

  Rais Xi Jinping wa China yuko ziarani nchini Afrika Kusini, baada ya kumaliza ziara yake nchini Senegal na Rwanda, na akiwa njiani kurejea China, atafanya ziara ya kirafiki nchini Mauritius.

  Senegal, ambayo ni nchi ya Afrika Magharibi, Rwanda, nchi ya Afrika Mashariki, Afrika Kusini ambayo iko kusini mwa Afrika, na Mauritius nchi ya kisiwa iliyoko Afrika Mashariki, zote ni nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na pia zimepata matokeo.

  Ingawa China na Afrika zina hali tofauti na viwango vya maendeleo ya uchumi na jamii ni tofauti, lakini zinaendana katika njia ya kujipatia maendeleo na ustawi. Nchi nyingi za Afrika zina nia kubwa ya kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia moja". Rais Macky Sall wa Senegal na rais Paul Kagame wa Rwanda, mara nyingi wamesema kuwa wanaunga mkono pendekezo hilo na kupenda kushiriki kwenye ujenzi wa mawasiliano.

  Nchi za Afrika zina hamu kubwa ya kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kwa sababu yamabadiliko ya mazingira ya ndani na nje ya nchi. Mabadiliko ya nje ya nchi hizo ni pamoja na nchi za Ulaya na Marekani kupunguza uwepo wao kimkakati barani Afrika, na hivyo nchi za Afrika sasa zinaangalia mashariki. Pia, katika mageuzi ya miundo ya uchumi, nchi za Afrika zina shinikizo kubwa na matarajio yao kwa China yanaongezeka, na mwisho, nchi za Afrika zinataka kutumia pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kutimiza maendeleo ya viwanda.

  Afrika inashiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa kuwa pendekezo hilo lina msingi mzuri wa ushirikiano. China na Afrika ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, mawazo ya maendeleo ya kila upande yanaendana, na mipango ya maendeleo inaweza kuunganishwa. Katika mipango iliyopo sasa ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kuna mambo ya mawasiliano ya miundo mbinu, kwa mfano ujenzi wa pamoja wa mitandao ya reli ya kasi, barabara kuu na safari ya anga ya kikanda barani Afrika. Pia Afrika kwa upande wake inawasiliana na China, kwa mfano, ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika inataka kutimiza utandawazi wa viwanda, na China ni nguvu kubwa ya kutegemewa na Afrika.

  Afrika imekuwa sehemu muhimu isiyokosekana ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na pia baada ya juhudi za miaka mingi itakuwa sehemu yenye mafanikio makubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako