• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda na Japan zakubaliana kuanza mradi wa barabara

    (GMT+08:00) 2018-07-24 19:21:45
    Serikali ya Uganda na ile ya Japan zinakamilisha mazungumzo ya kuanza ujenzi wa daraja la New Nile mjini Kampala.

    Mwakilishi wa shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japana JICA nchini Uganda

    Fukase Yutaka, amesema wanatarajia kuanza ujenzi wa daraja hilo mwishoni mwa mwaka huu.

    Mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ukipitia Kibuli, Nsambya na mzunguko wa Mukwano kwenye awamu ya kwanza, huku nayo awamu ya pili ikipitia maeneo ya Kitgum , Garden City barabara ya Jinja.

    JICA ilipata kandarasi ya mradi huo miaka 8 iliopita ikiwa ni mpango wa serikali wa kuondoa msongamano wa magari kwenye mji mkuu Kamapala.

    Utagharimu shilingi bilioni 659 na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 36.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako