Katibu wa kudumu kwenye wizara ya fedha Caleb Rwamuganza, akisaini uanachama wa jukwaa hilo amesema litaisaidia Rwanda kutekeleza miradi kadhaa ya miundo msingi.
Miradi inayolengwa na Afrika 50 ni kama vile, uchukuzi na kawi ambayo inahitajika kwa asilimia 70 kati ya sasa na mwaka 2025.
Mkurungezi mkuu wa Africa 50 Alain Ebobisse amesema jukwaa hilo linaleta pamoja washirika kwenye sekta ya uma na ile ya kibinafsi kufadhili miradi ya maendeleo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |