• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri wa Mifugo aunda Kanda za Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali

    (GMT+08:00) 2018-07-24 19:22:20
    Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Luhaga Mpina ameunda Kanda za Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, ikiwemo ya Ziwa Victoria na kuteua maofisa wapya watakaokuwa na jukumu la kudhibiti na kutokomeza uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Victoria ifikapo Desemba, mwaka huu.

    Waziri Mpina amemteua Didas Mtambalike kuwa Mkuu mpya wa Kanda mpya ya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Victoria.

    Pia ameunda kanda mbili za kiulinzi za Sengerema na Ukerewe.

    Serikali pia imeanzisha Kituo cha Ukaguzi wa Mazao ya Uvuvi mkoani Singida na kuweka vizuizi katika maeneo yote yaliyoripotiwa kuwepo matukio ya utoroshaji wa rasilimali za uvuvi hapa nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako