• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Magufuli apokea bilioni 736 kutoka mashirika ya umma

    (GMT+08:00) 2018-07-24 19:23:00
    Rais John Magufuli wa Tanzania amepokea hundi za Sh bilioni 736.36 kutoka kampuni, wakala, taasisi na mashirika ya umma 43, ikiwa ni gawio kwa serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

    Rais alipokea gawio hilo jijini Dar es Salaam kutoka kwa kampuni na mashirika hayo, ambayo serikali ina hisa zake au inamiliki kwa asilimia 100 alisema, fedha hizo zinatarajiwa kuwezesha serikali kuendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

    Magufuli alimuagiza Msajili wa Hazina, Athuman Mbuttuka, kuhakikisha mashirika yote yanatoa gawio kwa serikali, na yatakayoshindwa uongozi wake ubadilishwe au mashirika hayo yafutwe.

    Alisema katika miaka miwili gawio limeongezeka, lakini kiasi kinachopatikana bado ni kidogo sana ikilinganishwa na uwekezaji uliofanyika.

    Serikali iliwekeza zaidi ya Sh trilioni 49.05 kwenye taasisi na kampuni mbalimbali, lakini baadhi ya mashirika hayajakabidhi mgao wao kwa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako