Aidha, taakwimu kutoka kwa kituo cha kimataifa cha biashara zinaonyesha kuwa mauzo ya Kenya kwenye soko la Uingereza yamepungua kutoka shilingi bilioni 50 mwaka 2009 hadi bilioni 37 mwaka 2017.
Taasisi hiyo imesema mauzo kwenye soko hilo kutoka kote duniani yameongezeka kwa asilimia 15 mwaka 2017.
Mwaka huo wa 2017 kenye ilikuwa imepoteza mgao wake wa soko la Uingereza wa bidhaa zake tatu kuu kwa nchinyingine.
Mkuu wa utafiti kwenye shirika la maendeleo ya kiuchumi Dirk Wellem Te Velde amesema Kenya imepoteza ushindani wake na hivyo inahitaji kuongeza kampeni za kukuza tena mauzo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |