• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti wagundua mfumo unaosababisha aleji (mzio) wa chakula wa watoto

  (GMT+08:00) 2018-07-25 08:16:36

  Utafiti mpya wa Marekani umeonesha kuwa kemikali kwenye tishu za maji za watoto wachanga zinaweza kuharibu sehemu ya juu ya ngozi. Kama watoto hao wanabeba mabadiliko ya jeni ya uharibifu wa ngozi, kugusa kemikali hiyo kunaweza kuongeza hatari ya kupata aleji (mzio) wa chakula.

  Watafiti kutoka chuo kikuu cha Northwestern cha Marekani na chuo kikuu cha Indiana cha Marekani wamesema, kubeba mabadiliko husika ya jeni, kugusa kemikali kwenye tishu za majimaji za watoto wachanga na kugusa chanzo cha mzio wa chakula kunasababisha mchakato wa mzio wa chakula kwenye kipindi cha watoto na ujana.

  Kwenye jaribio, watafiti hao waliwafanya panya wachanga kugusa kemikali zilizopo kwenye tishu za majimaji na kuwafanya kugusa chanzo cha mzio wa chakula na vumbi mara tatu hadi nne ndani ya wiki mbili. Baada ya hapo panya hao walipokula yai au karanga, walipata mzio kwenye ngozi na tumbo.

  Watafiti hao wameeleza kuwa ngozi ya juu iliundwa na lipide, kemikali zilizopo kwenye tishu ya majimaji zinaweza kuharibu lipide hizo. Kama watoto wakibeba mabadiliko ya jeni za uharibifu wa ngozi, kugusa vitu hivyo kutaongeza hatari ya kupata mzio wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako