• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yaanza kambi kwa ajili ya mashindano ya vijana mwezi ujao

  (GMT+08:00) 2018-07-25 09:06:06

  Timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa mpira wa mikono ya vijana chini ya miaka 20 imeingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika huko huko nchini Rwanda kuanzia Agosti 8 hadi Agosti 12 mwaka huu.

  Licha ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo, Rwanda walilazimika kufuzu kwa njia ya mtoano ambapo waliifunga Uganda kwa alama 32:27 kwenye mashindano ya kanda ya tano yaliyofanyika Uganda.

  Timu za mataifa 12 ya Afrika zinatarajiwa kushindana mwezi ujao nchini Rwanda, na timu mbili zitakazoibuka mabingwa kutokana na mpangilio wa Umri zitafuzu mashindano ya dunia yatakayofanyika mwakani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako