• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Shule za Sekondari nchini Kenya yafunguliwa jana

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:06:45

    Mashindano ya michezo kwa shule za sekondari nchini Kenya yamefunguliwa jana, ambapo kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete (netiboli), miongoni mwa mechi zilizochezwa mabingwa watetezi Kaya Tiwi kutoka mkoa wa Pwani walipata ushindi wa alama 42-30 dhidi ya Syumile kutoka kaunti ya Makueni.

    Jambo la kufurahisha na la kipekee katika mechi hiyo ya kundi B, alama zote 42 za Kaya Witi zilipatikana kupitia ndugu wa familia moja waliocheza kwa ustadi mkubwa, Melda Oguda aliyefunga 22 na Monica Oguda aliyefunga 20.

    Katika mechi moja ya kundi A, Nyakachi Girls kutoka mkoa wa Nyanza ilipata ushindi mnono wa alama 60-15 dhidi ya Olympic Mixed ya Nairobi, na katika kundi C, Karuri kutoka mkoa wa Kati walishinda kwa alama 36-34 dhidi ya St. Monica Bukokholo kutoka mkoa wa Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako