• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Nigeria akana kupokea dola 1,000

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:08:51

    Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Nigeria Salisu Yusuf amekana tuhuma za kupokea rushwa zilizoelekezwa kwake, licha ya mkanda wa video unaomuonyesha akipokea fedha inayodaiwa kuwa ni kiasi ya dola za kimarekani 1000 kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwake kuwa ni wakala wa wachezaji.

    Inadaiwa kuwa Salisu alipokea fedha hizo ili kuorodhesha wachezaji wawili kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichokuwa kinashiriki mashindano ya Afrika mwaka 2018 kwa wachezaji wa ligi za ndani na akiahidiwa kupewa nyongeza ya asilimia 15 nyingine endapo wachezaji hao wawili watacheza.

    Sakata hili la kocha Salisu ni mwendelezo wa uchunguzi wa vitendo vya rushwa kwenye soka la Afrika unaofanywa na mwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremeyaw Anas, ambaye katika mkasa huu alimtuma mwandishi mwenzake aliyejifanya ni wakala wa wachezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako