• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu kumi wafariki dunia kutokana na mvua kubwa na mafuriko Sudan

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:14:14

    Habari kutoka gazeti la Sudan Tribune imesema mvua kubwa na mafuriko yametokea katika maeneo tofauti nchini Sudan, na kusababisha vifo vya watu kumi.

    Ripoti hiyo imesema watu wasiopungua saba wamefariki dunia na wengine watatu hawajulikani walipo kutokana na mvua kubwa na mafuriko yaliyotokea kaskazini na kaskazini mashariki mwa mji wa al-Nuhood, Kordofan Magharibi.

    Mashuhuda wamesema mvua kubwa na mafuriko yamesababisha nyumba kati ya 1,500 hadi 2,000 kubomoka. Wahanga watatu kati yao ni wafungwa waliokuwa ndani ya gereza la mji huo, ambalo pia limeporomoka.

    Gavana wa jimbo la Kordofan Magharibi Bw Ahmed Ajab Al-Fiya ametoa amri kwa mamlaka yote husika kuchukua hatua za afya na ulinzi, ili kukabiliana na mvua na mafurko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako