• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • COMESA yatuma ujumbe wa waangalizi kwa ajili ya uchaguzi nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:30:07
    COMESA yatuma ujumbe wa waangalizi kwa ajili ya uchaguzi nchini Zimbabwe

    Soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) jana limesema, limetuma ujumbe wa waangalizi wa muda mfupi nchini Zimbabwe kwa ajili ya uchaguzi wa nchi hiyo utakaofanyika tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu.

    Ujumbe huo umeundwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa COMESA, ambao unaongozwa na mwanachama wa Kamati ya Wazee ya COMESA Bw. Ashraf Gamal Rashed.

    Taarifa iliyotolewa na COMESA inasema, ilituma ujumbe huo kutokana na mwaliko wa serikali ya Zimbabwe kupitia tume yake ya uchaguzi. Taarifa hiyo pia imesema, ujumbe huo utafuatilia maandalizi ya uchaguzi, na kufanya majadiliano na pande husika. Lengo la ujumbe huo ni kukusanya habari kuhusu uchaguzi na kutathmini maandalizi ya uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako