• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Tanzania wapiga marufuku magari chakavu elfu 33 ili kuzuia ajali

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:55:05

    Jeshi la polisi Tanzania limepiga marufuku magari zaidi ya elfu 33 ikiwa ni pamoja na mabasi, katika kampeni ya nchi nzima kukabiliana na ajali.

    Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Bw. Fortunatus Musilimu amesema kwenye ukaguzi uliofanyika kwenye magari zaidi elfu 81, magari zaidi ya elfu 33 yalikutwa na dosari. Madereva na wamiliki wa magari 25 walifikishwa mahakamani kutokana na kuendesha magari mabovu.

    Kamanda Musilimu pia amesema kuanzia wiki ijayo madereva wa magari ya huduma kwa umma watatakiwa kubeba vyeti vya shule za udereva, ili kuwatambua madereva wazembe.

    Hatua zinazochukuliwa na jeshi la polisi la Tanzania zinatokana na mfululizo wa ajali za barabarani zilizotokea mwezi juni na kusababisha vifo vya watu wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako