• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya imekamata bidhaa feki zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 75 ndani ya miezi miwili

    (GMT+08:00) 2018-07-25 09:55:55

    Serikali ya Kenya imesema imekamata bidhaa feki zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 75 kwenye kampeni iliyofanyika nchi nzima katika kipindi cha miezi miwili. Naibu mkuu wa utumishi wa umma Bw. Wanyama Musiambo ameahidi kuimarisha kampeni dhidi ya bidhaa feki na biashara haramu.

    Amesema bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na sukari haramu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 53, sigara zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 8.2, bidhaa za kilimo zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3.4, vifaa vya umeme vya nyumbani vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3 na pombe yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2.7.

    Bw. Musiambo amesema bidhaa feki ni hatari kwa afya ya watumiaji, na zinakwamisha maendeleo ya sekta ya uzalishaji, ambayo ni moja ya ajenda muhimu za maendeleo manne makubwa ya rais Uhuru Kenyatta, yaani Big Four.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako