• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chuo kikuu cha Witwatersrand chasema ushirikiano kati yake na China umeshuhudia maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini katika sayansi na elimu

  (GMT+08:00) 2018-07-25 14:42:38

  Chuo kikuu cha Witwatersrand kikiwa ni chou kikuu maarufu nchini Afrika Kusini na katika bara zima la Afrika, kinaongoza kwenye utafiti wa sayansi na teknolojia nchini Afrika Kusini, na kimetekeleza miradi mingi ya ushirikiano kati ya Afrika Kusini na China katika utafiti wa sayansi na teknolojia.

  Ofisa anayeshughulikia mambo ya China katika chuo kikuu cha Witwatersrand Bibi Yang Yan amesema, hadi sasa chuo kikuu kimeandaa wahitimu wapatao 700 kutoka China, na pia kuna wasomi sita wa China wanafundisha katika chuo kikuu hicho. Amesema huu ni mwaka wa 20 tangu China na Afrika zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, na ushirikiano wa sayansi na teknolojia kati ya chuo kikuu hicho na China umeshuhudia maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini katika sayansi na elimu.

  Katika miaka mitano iliyopita, wizara za sayansi na teknolojia za nchi hizo mbili zimeimarisha ushirikiano kupitia kujenga maabara na kituo cha pamoja cha utafiti, hatua ambazo zimetia msukumo mkubwa kwa ushirikiano kati ya watafiti wa pande hizo mbili.

  Bibi Yang Yan amesema hivi sasa chuo kikuu cha Witwatersrand kimekuwa na ushirikiano na vyuo vikuu vya China kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo uchimbaji madini, utafiti wa binadamu na viumbe wa kale, nishati, fizikia, Big data, na matibabu na afya. Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, katika nusu ya pili ya mwaka huu chuo kikuu hicho pia kitaanzisha ushirikiano na chuo kikuu cha madini cha China kuhusu matumizi ya mfumo wa satelaiti za kuongoza mawasiliano ya ardhini za Beidou.

  Bibi Yang Yan ameongeza kuwa mbali na ushirikiano na vyuo vikuu vya China, Chuo kikuu cha Witwatersrand pia kimeshirikiana na makampuni ya sayansi na teknolojia ya China, ikiwemo kampuni ya Tehama ya Huawei na kampuni ya dawa ya Tongrentang, na miradi mingi ya ushirikiano huo imetambuliwa na kusifiwa na jamii za huko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako