• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza mpango wa nchi mbili ni njia msingi wa kututua suala la Israel na Palestina

    (GMT+08:00) 2018-07-25 19:15:05

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, mpango wa nchi mbili ni njia ya kimsingi ya kutatua suala la Israel na Palestine, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kushikilia maazimio ya Umoja wa Mataifa na kuongeza nguvu katika kuanzisha tena mazungumzo ya amani.

    Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, Bw. Ma amesema, pande zote zinatakiwa kutekeleza azimio namba 2334 la baraza hilo, kusimamisha ujenzi wa makazi kwenye eneo linalodhibitiwa na kuharibu makazi na mali ya wapalestina na kuchukua hatua kuzuia vitendo vya kimabavu dhidi ya raia.

    Bw. Ma amesema, China daima inaunga mkono nchi huru ya Palestina yenye mipaka iliyoamuliwa mwaka 1967, ambapo mji mkuu wake ni Jerusalem ya mashariki, na kushiriki zaidi kwenye mambo ya jumuiya ya kimataifa. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za kikanda kuongeza mawasiliano ya kimkakati, kusaidia kulinda amani, utulivu na haki ya Mashariki ya Kati

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako