• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuajiri wataalamu katika miradi mbalimbali inayoendelea

    (GMT+08:00) 2018-07-25 19:28:26
    Serikali kwa kushirikiana na taasisi ya sekta binafsi Tanzania ,TPSF,imeanzisha mkakati mpya wa kuibua wataalamu wapya watakaoajiriwa kwa kuanzisha mabaraza ya ujuzi ya kisekta ambayo yatafanya kazi ya kuwapa mafunzo wataalamu hao.

    Akizungumza katika mkutano wa wakurugenzi kutoka taasisi mbalimbali ambazo ni wanachama wa TPSF,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ,Godfrey Simbeye,alisema katika miezi miwili iliyopita,wameanza kuzungumza na wadau mbalimbali nchi nzima kwa ajili ya kuanza mchakato huo.

    Simbeye alisema kazi hiyo walipewa na serikali kuhakikisha wanajenga ujuzi kwa watanzania wengi ,ili kuwawezesha kupatikana wataalamu wazuri watakaoajirika hususan katika miradi mbalimbali inayoendelea nchini humo katika kufanikisha kufikia Tanzania ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

    Alisema katika kufanikisha mkakati huo,tayari serikali imekopa U$125milioni (Tshs285 bilioni) kutoka Benki ya Dunia ambazo zitasaidia kutekeleza mkakati huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako