Bei za parachichi ulaya zimeshuka kwa zaidi ya nusu kutokana na kuongezeka kwa bidhaa hiyo haswa kutoka Peru na Afrika Kusini.
Mfuko wa kilo nne wa parachichi ulizwa kwa kati ya Sh471.88 na Sh589.85 (€4 and €5) ikilinganishwa na bei ya kati ya Sh1,297.67 — Sh1, 533.61) mwaka jana.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Wazalishaji Mazao Safi Okisegere Ojepat amesema bei hizo za chini zimewaumiza wakulima kwa sababu mvua iliyonyesha kwa kipindi kirefu ilifanya zao hilo kuchelewa kukomaa na hatimaye kuvuna sawa na wakulima wa Peru.
Akizungumza kwa njia ya simu Ojepat alisema sasa wanatafuta masoko mapya katika Mashariki ya mbali.Alielezea imani yake kwamba China na India zitafungua milango.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |