• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatoa ruzuku kwa wakulima, huku ikipinga nchi nyingine kutoa ruzuku

    (GMT+08:00) 2018-07-25 19:42:35

    Rais Donald Trump wa Marekani jana amesema Marekani itatoa ruzuku ya dola za kimarekani bilioni 12 kwenye sekta ya kilimo , ili kuwasaidia wakulima wa Marekani kukabiliana na vita ya kibiashara kati ya nchi hiyo na China, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine.

    Awali, Marekani ilisema sababu yake ya kuanzisha vita ya kibiashara ni bidhaa zinazoingia Marekani zimepata ruzuku ya kiserikali. Lakini sasa Marekani imeanza kutoa ruzuku. Kitendo hiki kimethibitisha onyo lililotolewa na wataalamu wa uchumi dhidi ya Marekani, kuwa hakuna mshindi kwenye vita ya kibiashara, kila upande utapata hasara.

    Serikali ya Marekani kutumia fedha kubwa kutoa ruzuku ya kilimo, ni matokeo ya lazima ya hatua ya Marekani kutoza ushuru kwa wenzake wa kibiashara na pande nyingi kulipiza kisasi. Sekta ya kilimo ya Marekani ni lengo kuu la hatua za kupiga kisasi za nchi mbalimbali. Wakulima wa Marekani walitolewa kafara kwenye vita ya biashara vilivyoanzishwa na serikali ya nchi hiyo, na wanaathirika na matokeo ya sera ya ushuru ya nchi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako