• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kujitoa kwenye mwelekeo mbaya kuhusu nyongeza ya ushuru

    (GMT+08:00) 2018-07-25 20:31:22

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, hakuna mshindi katika vita ya kibiashara, na kuitaka Marekani kutoka kwenye mwelekeo mbaya na kutoendelea na hatua za nyongeza ya ushuru.

    Amesema mvutano wa kibiashara unaochochewa na Marekani hautapata faida yoyote, bali utakuwa kikwazo kwa kila mtu. Ameitaka Marekani kusikiliza sauti ya busara ndani ya nchi na kujitoa kwenye mwelekeo mbaya.

    Serikali ya Marekani imetangaza kuwa itatoa dola bilioni 12 za Kimarekani kama ruzuku kwa wakulima nchini humo wanaoathiriwa na mvutano wa kibiashara unaoendelea sasa. hata hivyo wabunge na wakulima wanakosoa mpango huo, na kusema wakulima wanataka biashara zaidi kuliko ruzuku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako